← SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Waziri Wong aelekea katika kongamano lamawaziri wa mambo ya nje wa ASEAN kuimarisha uhusiano wa Australia na nchi wanachama artwork

Taarifa ya Habari:Waziri Wong aelekea katika kongamano lamawaziri wa mambo ya nje wa ASEAN kuimarisha uhusiano wa Australia na nchi wanachama

SBS Swahili - SBS Swahili
13:03
Play episode

Show notes

Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong anatarajiwa kwenda Ufilipino kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Asia Mashariki na Jukwaa la Kikanda la ASEAN. Tume ya Dhamana na Uwekezaji ya Australia inasema imepata rekodi ya dola milioni 830 katika amri za adhabu za kiraia wakati wa Mwaka wa Fedha wa 2025-2026. Tume hiyo ilianzisha chunguzi zaidi ya 250, ambazo zilisababisha hatia 25 za jinai na watu 11 kuhukumiwa kifungo cha gerezani. Karibu watu 930 wamefariki dunia kutokana na Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hii ikiwa ni kulingana na Wizara ya afya nchini humo. Vifo hivyo vimerekodiwa miongoni mwa visa 2,344 vya maambukizi vilivyothibitishwa hadi siku ya Jumamosi imesema wizara hiyo hii leo. Vifo vipya vilirekodiwa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, idadi ya juu kabisa kuwahi kurekodiwa kwa siku moja. Meli ya mafuta yenye bendera ya Tanzania imetekwa nyara na maharamia wanaoshukiwa kuwa wa Somalia katika pwani ya Yemen, vimebaini vyanzo vya usalama na maafisa wa eneo hilo kuhusu tukio hilo. Meli hiyo imehamishwa hadi majini katika eneo la Bari kaskazini mashariki mwa Somalia, kulingana na maafisa wa eneo hilo.

More from this show

More
  1. How laws are made, and how they affect you | How Australia Works - Jinsi sheria zinavyotungwa, na jinsi zinavyokuathiri | Jinsi Australia Inavyofanya kazi.

    How are laws made in Australia? Through Wurundjeri Elder Uncle Dave Wandin’s story of the Birrarung, also known as the Yarra River, learn how an idea becomes a bill, passes through…

    09:31
  2. Taarifa ya Habari:Zaidi ya wafanyakazi 460,000 wanatarajiwa kupata ongezeko la mishahara kwa ajili ya usawa wa kijinsia

    Zaidi ya wafanyakazi 460,000 wa afya, ulemavu na huduma za jamii wa Australia wanatarajiwa kuongezwa mishahara, wakati Serikali ya Shirikisho ikitangaza kifurushi cha ufadhili cha…

    15:36
  3. Makala Leo:Wajibu wa Huduma katika Nyanja ya Kidijitali: Greens wataka mamlaka ya kushtaki makampuni makubwa ya teknolojia

    Wakati Bunge likijiandaa kujadili Muswada uliopendekezwa wa Wajibu wa Huduma ya Kidijitali, chama cha Greens kinataka sheria hizo ziende mbali zaidi kwa kuruhusu Waaustralia kuzish…

    08:02
  4. Birth and pregnancy care options in Australia - Australia Yafafanuliwa:Chaguzi za huduma ya uzazi na ujauzito nchini Australia

    If you're first-time parents in Australia, choosing where and how to give birth can feel overwhelming. Whether you go through the public or private health system, it is important t…

    14:07
  5. Taarifa ya Habari:Australia yajiandaa kwa msimu hatari wa moto wa msituni unaosababishwa na "super El Niño"

    Australia inajiandaa kwa kile kinachotarajiwa kuwa msimu hatari wa moto wa msituni unaosababishwa na tukio linaloitwa "super El Niño" pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.

    14:31
  6. Breast screening: What to expect and why it matters - Australia Yafafanuliwa: Uchunguzi wa saratani ya matiti: Nini cha kutarajia na kwa nini ni muhimu

    Regular breast screening can help find breast cancer early, before you notice any signs or symptoms. Screening is free for eligible women or people at risk of breast cancer. It tak…

    14:21
Now Playing
Taarifa ya Habari:Waziri Wong aelekea katika kongamano lamawaziri wa mambo ya nje wa ASEAN kuimarisha uhusiano wa Australia na nchi wanachama — SBS Swahili - SBS Swahili | Podcast | Josplay Music